Watumiaji

Mtumiaji wa Mfumo wa SIS katika ngazi ya Shule

Mkuu wa Shule

Baada ya Mkuu wa Shule kusajiliwa na Afisa wa TEHAMA wa Halmashauri, yafuatayo ndio majukumu yake:-

  1. Kusajili na kusimamia watumiaji katika ngazi ya shule.
  2. Kugawa majukumu kwa watumiaji
  3. Kutengeneza mikondo
  4. Kuopanga walimu kwa madarasa.
  5. Kupanga walimu kwa Masomo
  6. Masomo kwa Madarasa

Mwalimu wa Darasa

Baada ya Mwalimu wa Darasa kusajiliwa na kupangiwa majukumu na Mkuu wa Shule, yafuatayo ndio majukumu yake:-

  1. Kuangalia na kuhakiki orodha ya wanafunzi katika darasa alilopangiwa.
  2. Kupanga wanafunzi katika mikondo iliyotengenezwa na Mkuu wa Shule na kupangiwa yeye.
  3. Kuchukua mahudhurio ya wanafunzi.

Angalizo

Mkuu wa shule ataweza kufanya majukumu yote kama baada ya kutengenezewa akaunti na Afisa TEHAMA wa Halmashauri