Jinsi ya kutengeneza mkondo

Baada ya kufanikiwa kusajili na kuwapangia majukumu watumishi katika ngazi ya shule, Mkuu wa Shule anatakiwa kutengeneza mikondo ya madarasa kwa kubofya menyu iliyoandikwa shule inayopatikana upande wa kushoto mwa ukurasa wake na kisha kubofya menyu ndogo ya tengeneza mikondo Kufanikisha utengenezaji wa mikondo utamuwezesha Mkuu wa Shule kuweza kupanga walimu kwa madarasa, masomo kwa madarsa na walimu kwa masomo. Utengenezaji wa mikondo ni kama inavyoonekana hapa;

alt Imange Description

Panga masomo kwa madarasa

Bofya menyu iliyoandikwa Shule na kisha bofya menyu ndogo iliyoandikwa Masomo ya Madarasa na kisha utafunguka ukurasa utakao kuwezesha kupanga masomo kwa madarasa kama inavyoonekana;

alt Imange Description

Panga walimu kwa madarasa

Bofya menyu iliyoandikwa Watumishi na kisha bofya menyu ndogo iliyoandikwa Walimu kwa Madarasa na kisha utafunguka ukurasa utakao kuwezesha kupanga walimu kwa madarasa kama inavyoonekana;

alt Imange Description

Panga walimu kwa masomo

Bofya menyu iliyoandikwa Watumishi na kisha bofya menyu ndogo iliyoandikwa Walimu kwa Masomo na kisha utafunguka ukurasa utakao kuwezesha kupanga walimu kwa masomo kama inavyoonekana;

alt Imange Description