Mwalimu wa Darasa
Namna ya kuingia kwenye mfumo
Baada ya kusajiliwa na Mkuu wa Shule, anza kwa kufungua kivinjari chako katika kompyuta ambacho kimeunganishwa katika mtandao wa internet. Kivinjari hicho kinaweza kuwa Google Chrome, Mozila Firefox au Microsoft Edge.
Kisha aandika anuani ifuatayo sis.tamisemi.go.tz. Anza kwa kuingiza “Username” na “Password” uliyotengenezewa na Mkuu wa Shule. Kisha Bofya kitufe kilicho andikwa “INGIA” ili uweze kuingia kwenye mfumo.
Mara baada ya mfumo kufunguka kwa mara ya kwanza utatokea ukurasa unaokutaka kubadilisha neno la siri. Andika neno la siri (Default Password) ambayo ni secret, kisha andika neno jipya la siri na kulihakakiki. Baada ya hapo Hifadhi taarifa zako. Mfumo utakuotoa nje na kukutaka uingie tena, weka barua pepe na nywila mpya kisha bofya kitufe kilichoandikwa ingia.
Mara baada ya mfumo kufunguka kwa mara ya kwanza huu ndio utakuwa ukurasa wa kwanza unaoonyesha menyu zitakazofanyiwa kazi na Mwalimu wa Darasa.
Panga Wanafunzi kwenye Mikondo
Baada ya kupewa majukumu ya Mwalimu wa Darasa yaani Class Teacher na kupangiwa darasa na Mkuu wa Shule Mwalimu wa Darasa ataanza kupanga wanafunzi kwenye mikondo aliyopangiwa na Mkuu wa Shule na kisha atabofya kitufe kilichoandikwa HIFADHI kama inavyoonekana hapa;
Orodha ya Wanafunzi kwenye mkondo
Mwalimu wa Darasa anaweza kuangalia orodha ya wanafunzi waliopangwa kwenye mkondo kama inavyoonekana;
Orodha ya Wanafunzi
Mwalimu wa Darasa pia anaweza kuangalia orodha ya wanafunzi kama inavyoonekana hapa;
Chukua Mahudhurio ya Wanafunzi
Mwalimu wa Darasa anajukumu la kuchukua mahudhurio ya wanafunzi katika darasa husika kwa kipindi/ muda wa masomo (Asubuhi/Mchana). Katika mchakato wa kuchukua mahudhurio Mwalimu wa Darasa anao uwezo wa kuweka sababu kwa wanafunzi wote ambao watakuwa hawajafika/ kuhudhurio kipindi hicho. Kutokana na baadhi ya madarasa kuwa na wanafunzi wengi, mfumo unamuwezesha Mwalimu wa Darasa kuweza kuweka alama ya TICK kwenye kichumba kilichowekewa alama ya namba 4 ili kuweza kuonyesha kwamba wanafunzi wote wapo na baada ya hapo kuanza kuondoa alama hiyo kwa wale ambao hawapo sambamba na kuweka sababu kama inavyoonekana hapa;
Baada ya kuchukua mahudhurio Mwalimu wa Darasa atatakiwa ahifadhi mahudhurio hayo kama inayoonekana hapa;
Hariri Mahudhurio
Mfumo unamuwezesha MWalimu wa Darasa kuweza kuhariri Mahudhurio kama inavyoonekana hapa;
Pangia Wanafunzi Masomo
Mfumo unamuwezesha Mwalimu wa Darasa kuwapangia wanafunzi masomo kama inavyoonekana hapa;
Wanafunzi Waliopangiwa Masomo
Mfumo unamuwezesha Mwalimu wa Darasa kuangalia wanafunzi waliopangiwa masomo kama inavyoonekana hapa;
Mwisho wa Moduli ya Mahudhurio