Utangulizi

Mfumo wa Taarifa za Shule (School Information System - SIS) ni mfumo unaotumika kukusanya taarifa za shule na kusimamia shughuli za uendeshaji na usimamizi wa shule. Mfumo huu wa SIS unatumika kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya elimumsingi kuanzia ngazi ya shule, kata, halmashauri na mkoa.

Watumiaji wa mfumo huu ni watumishi ambao ni Walimu na wale ambao sio Walimu katika ngazi ya Shule, Afisa Elimu kata kwa ngazi ya Kata, idara ya Elimu ngazi ya Halmashauri, idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wizara na Wadau wa maendeleo.

Mfumo huu unapatikana kwa njia zifuatazo:-

  1. Mobile APP inayoitwa SIS Tanzania ambayo inapatikana kwenye Playstore (Android).
  2. WEB ambayo inapatikana kwa anuani ifuatayo SIS Tanzania

alt Imange Description

Moduli ya Mahudhurio (Attendance)

Moduli ya Mahudhurio ni moduli katika mfumo huu wa Taarifa za Shule (SIS). Moduli hii inawezesha kuchukua mahudhurio ya walimu na wafanyakazi wasio walimu katika ngazi ya shule sambamba na kuchukua mahudhurio ya wanafunzi kwa vipindi husika.